David Bright: Botswana imekuja ikiwa tofauti.

Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Soka ya Botswana David Bright amelishukuru Shirikisho la Soka nchini 'TFF' kwa namna ambavyo wameipokea timu kuelekea mchezo wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars.

Bright amesema wamekuwa na safari ya kusuasua toka wameondoka Botswana hadi imewalazimu kupumzika leo kutofanya mazoezi, lakini kwa namna walivyopokelewa na TFF imewapa nguvu ya kupambana katika mchezo huo.

Meja huyo Mstaafu wa Jeshi la Botswana amesema hawajiandaa sana ukizingatia kuwa timu yao bado ni mpya lakini wataleta upinzani mkali katika mchezo huo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru.

-Mimi ni kocha mpya hapa, nimefanya mabadiliko kwenye kikosi, kuna sura nyingi mpya na nimekuja na falsafa tofauti kuanzia muonekano mpaka mambo ya kiufundi, kikosi hiki ni kipya kabisa na kile kilichocheza hapa Machi, tutatoa Changamoto mpya" Alisema kwa kuongezea yale aliyoyasema awali.

Kikosi cha Botswana. 

Botswana imekuja na wachezaji 18 wakiwamo makipa Mampule masule, Noah Maposa na Antony Gouws. mabeki ni Letsweletse, Mosha Gaolaolwe, Simisane Mathumo, Thabang Mosigi, Lesenya Ramorake, Tapiwa Gadibolae na Bokani Leeton.

Viungo ni Alphonse Modisaotsile, Maano Ditshupo, Katlego Masole, Gift Moyo, Segolame Boy, Lemponye Tshireletso, Thero Setsile, Kabelo Seakanyeng,Jackson, Lemogang maswena.

Washambuliaji ni Tumisang Orebonye, Jarome Ramathakwane, Tebogo Sembowa, Hendric Moyo na Boipelo Oaitse.