CECAFA 2017: Tarehe yafahamika, Zimbabwe na Libya waalikwa.

Mashindano ya 39 ya kombe la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yanatarajiwa kufanyika jijini Nairobi nchini Kenya, kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 9 mwaka huu, imefahamika.

Mashindano hayo yanashirikisha nchini wanachama 12 na mwaka huu timu za taifa za Zimbabwe na Libya zimealikwa kama wageni kushiriki. 

Mwaka jana mashindano hayo hayakuandaliwa baada ya wenyeji Sudan kujiondoa na kisha Kenya iliyochukua nafasi ya kuandaa nayo kujiondoa dakika za mwisho.

Washiriki. 

Nchi zitakazoshiriki ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Sudan kusini, Djibouti, Eritrea, Somalia, Zimbabwe [wageni] na Zanzibar.

READ: CECAFA: COSAFA champs accept invitation to Kenya