ASFC: Hii hapa ratiba ya robo fainali

Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi Machi katika viwanja vinne tofauti nchini.

Ijumaa Machi 30, 2018 kutakuwa na mchezo mmoja katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ambapo wenyeji Stand United watawakaribisha Njombe Mji mchezo utakaoanza saa 10 kamili jioni.

Machi 31, 2018 kutakuwa na michezo miwili, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania saa mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 8 mchana Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Huku siku hiyo hiyo saa 2 kamili usiku Azam FC watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Jumapili Aprili Mosi, 2018 kutakuwa na mchezo mmoja, Singida United watakuwa wenyeji wa Dar Young Africans katika uwanja wa Namfua mjini Singida mchezo utakaonza saa majira ya saa 10 jioni.

Ikumbukwe bingwa wa michuano hiyo ataliwakilisha Taifa katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

NUSU FAINALI

Azam/Mtibwa v Stand/Njombe

Singida/Yanga v Prisons/JKT

(Mechi zitachezwa kati ya Machi 16 na 18)

FAINALI

Singida/Yanga/Prisons/JKT 

Vs 

Azam/Mtibwa/Stand/Njombe

(Mechi itachezwa kati ya Mei 30 na 31)