Tanzania yapanda viwango vya Ubora wa Soka Duniani.

Tanzania yapanda viwango vya Ubora wa Soka Duniani.

06 Jul 2017, 13:07

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), limetoa orodha ya viwango vya soka duniani kwa mwezi Julai huku Tanzania ikipanda kwa nafasi 25  kutoka nafasi ya 139 hadi nafasi ya 114 duniani huku ikishika nafasi ya 30 barani Afrika.

Hii inakuwa mara ya Pili kwa Tanzania kupanda kwa kasi ndani ya Miezi Michache kwani Ikumbukwe Katika viwango vilivyotoka Mwezi April Tanzania walipanda kwa Nafasi 22.

Hii ni kufuatia Tanzania kufanya vizuri katika michezo yake ya kimataifa ikiwemo mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika Ambapo Tanzania walitoka sare ya bao 1-1 na  Lesotho katika mchezo ambao ulifanyika Jijini Dar es Salaam mwezi uliopita. 

CECAFA.

Uganda wanaendelea kuongoza kanda ya Afrika Mashariki wakiwa  katika nafasi ya 74 , wakifuatwa na  Kenya ambao wako  katika nafasi ya 84 , Burundi ambao pia wamepanda kwa nafasi 27 wanashika nafasi ya 121 nao Rwanda ambao watacheza na Tanzania tarehe 15 mwezi huu katika mechi  ya  kufuzu michuano ya Mataifa  CHAN  mwaka 2019 itakayofanyika nchini Kenya, wakishika nafasi ya 127 wakati Ethiopia wakishuka hadi nafasi ya 136. 

Misri 

Misri wanaongoza kwa upande wa bara la Afrika wakifuatwa na Senegal ambao Wanashika nafasi ya pili  nao DR Congo wakishika nafasi ya tatu, Tunisia ya Nne na Cameroon ya tano.

Kwa dunia Ujerumani  inaendelea kushika nafasi ya  kwanza, Brazil ya pili ,Argentina ni ya tatu, Huku Ureno ikishika  nafasi ya nne nao Uswisi ikifunga tano bora kwa Upande Huo.

Related news
related/article
FIFA World Cup
The Iron Fist in Croatia's Velvet Glove
12 Jul 2018, 14:50
Kenya News
Ushuru, KCB clash to be aired live in NSL round 22
07 Jul 2018, 08:40
FIFA World Cup
World Cup Young Player award goes to Mbappe
3 hours ago
FIFA World Cup
First World Cup final own goal! Mandzukic makes history
5 hours ago
FIFA World Cup
Worlds Apart: Paul Pogba & Luka Modric
9 hours ago