SOREFA Kuzuia Uchaguzi Mkuu wa TFF, wataka watambulike Kama wajumbe.

SOREFA Kuzuia Uchaguzi Mkuu wa TFF, wataka watambulike Kama wajumbe.

11 Aug 2017, 22:14

Uongozi wa Chama cha Mpira wa miguu mkoa wa Songwe, umedhamiria kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini, endapo TFF itaendelea kuwa na msimamo wa kuwazuia wajumbe toka Songwe kuhudhuria na kupiga kura kwa madai Songwe sio Mkoa, katika Uchaguzi utakao fanyika Jumamosi ya Agosti 12 mkoani Dodoma.

Katika Taarifa ya Emmanuel Mwamlima ambaye ni Katibu Mkuu SOREFA, imesema kuwa Uongozi wa TFF unawazuia wajumbe wa Songwe kuhudhuria na kupiga kura kwa madai kuwa sio wanachama, kwa Maelezo kwamba mkoa huo haujaomba uanachama kwa maandishi, na hivyo Songwe Bado ni sehemu ya Mkoa wa Mbeya.

-Ukweli ni kwamba Songwe waliomba kwa barua ya tar 19/5/2017 na kupokelewa 22/5/2017, barua hiyo ikitanguliwa na barua ya 21/3/2016,iliyokuwa ikiitarifu TFF, kuanzishwa kwa chama kipya cha soka mkoa mpya wa Songwe, (SOREFA), barua Hiyo ni kutokana na kikao cha chama cha mkoa wa Mbeya (MREFA), ambacho kilihudhuriwa na mjumbe wa kamati ya utendaji, ya TFF Bwana Ayoub Nyenzi" Ilisema Sehemu ya Taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Aprili 22, 2016 SOREFA ilipata tangazo toka Kamati ya Uchaguzi ya TFF ikitaarifu ufanyike Uchaguzi wa viongozi wa mkoa mpya, tangazo ambalo lilisainiwa na makamu Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi TFF Domina Madeli. 

Uchaguzi wa SOREFA ulifanyika Disemba 3, 2016 kwa Mujibu wa Kanuni za uchaguzi za TFF.

Taarifa Ya Mwamlima imesema kwamba baadae SOREFA ilipokea barua ya kuteuliwa kwa Mkoa huo kuwa kituo cha ligi ya mabingwa wa mikoa, barua ambayo ilisainiwa na katibu mkuu wa TFF bwana Mwesigwa Selestine, ambapo Mabingwa wa mkoa wa Mbeya Boma FC walishiriki katika kituo hicho kama timu ngeni wakati mabingwa wa Songwe Green City walipangiwa kituo cha Tabora.

Wamehudhuria mkutano Mkuu. 

-Tarehe 6/6/2017 tulipata barua ya mwaliko kuhudhuria mkutano mkuu wa Uchaguzi, kama wajumbe halali barua iliyosainiwa na katibu mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine, lakini ajabu tarehe 4/8/2017 tukapata barua nyingine iliyo sainiwa na Madadi Salum ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu, kutualika Mkutanoni Kama wajumbe waalikwa" .

Taarifa hiyo imeendelea kusema "ukweli wa yote haya ni fitina za kiuchaguzi zinazofanywa na viongozi wanao Kaimu nafasi ya Rais Jamal Malinzi na Mwesigwa Selestine kwa maslahi ya Kaimu Rais wa TFF bwana Wares Kalia, juu ya madai yake kwamba wajumbe wa mkoa wa Songwe hawamuungi mkono hivyo, akaamua kuwatoa kibabe ili kupunguza idadi ya kura zinazo mpinga".

-Haya ni maonevu na matumizi mabaya ya madaraka, ambayo uongozi wa Songwe na wapenda haki popote Duniani hawawezi kuyakubali, Uongozi wa Songwe unasisitiza kwenda mahakamani kupinga nakudai haki yao" Iliendelea kusema taarifa hiyo.

Wajumbe wengine wa TFF. 

Aidha uongozi wa SOREFA umesema utaomba matokeo ya TAFCA , FRAT ,TWFA yabatilishwe kwakuwa wajumbe wa mkoa wa Songwe ambao hautambuliwi na TFF ya Wales Kalia, walishiriki Uchaguzi kuwachagua viongozi wavyama hivyo ambao watashiriki Uchaguzi wa TFF kesho.

-Taarifa za ndani ya kikao cha kamati ya utendaji ya TFF kilicho fanyika Leo Ijumaa, ambazo hazijathibitika, zinasema wajumbe walio wengi walikubaliana kuwa wajumbe wa Songwe waruhusiwe kupiga kura Kwani ni wajumbe halali lakini Karia na kundi lake walikataa katakata wakidai, swala hilo litaamuliwa na Leodigar Chila Tenga kesho jambo ambalo, liliwashangaza wajumbe, kwamba Tenga ataamua kama Nani?" Ilimaliza Taarifa hiyo ya Emmanuel Mwamlima. 

Related news
related/article
FIFA World Cup
Luka Modric: The Midfield Magician
11 Jul 2018, 19:20
Kenya News
Odhiambo ready for Sofapaka challenge
07 Jul 2018, 10:05
English Premier League
Mourinho's pre-season fears mount with Sanchez sidelined
2 hours ago
FIFA World Cup
World Cup Player Profile: Youri Tielemans
1 hour ago
English Premier League
Liverpool ace determined to stay
9 hours ago