waziri Harrison Mwakyembe: Tunataka uongozi usiokumbatia rushwa na ubadhirifu.

waziri Harrison Mwakyembe: Tunataka uongozi usiokumbatia rushwa na ubadhirifu.

12 Aug 2017, 11:41

Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, amewataka wajumbe wanaoshiriki uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Nchini TFF kuwachagua viongozi ambao wana maono ya kuimarisha na kuendeleza mpira wa miguu nchini. 

Akizungumza mapema Katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Saint  Gasper mjini Dodoma ambapo mkutano huo unapofanyika Mwakyembe, amewaomba wajumbe hao kuwachagua viongozi bora ambao wana dhamira njema na mpira wa nyumbani.

Viongozi wabadhirifu

-Viongozi bora huchaguliwa na wajumbe makini chagueni viongozi ambao wana dhamira njema viongozi ambao wana ari, moyo, weledi na uadilifu wa kuendeleza Soka letu viongozi ambao wana heshimu katiba na kudhamini uongozi wa pamoja", amesema Mwakyembe.

Pamoja na hayo Waziri huyo amewataka viongozi watakaochagukiwa kuisaidia Katika mipango ya kufanikisha maandalizi ya timu za Taifa kufanya vizuri Katika Mashindano ya kimataifa.

Upinzani 

Uchaguzi huo ambao unaendelea kwa sasa unatarajia upinzani mkali Katika nafasi ya urais ambapo wagombea sita wamejitokeza kugombea nafasi hiyo ya Jamal Malinzi ambaye hatawania nafasi hiyo kwa tuhuma za uadilifu wa fedha za TFF. 

Wanaowania Urais TFF ni pamoja na Kaimu Rais wa sasa, Wallace Karia, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Ally Mayay, Katibu wa zamani wa TFF Frederick Mwakalebela, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, Wakili Imani Madega, Msomi na Mwandishi wa Habari za Michezo wa zamani, Shija Richard na Katibu wa Klabu ya Mbeya City, Emmanuel Kimbe. 

Nafasi ya Umakamu wa Rais.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira Mkoa wa Dodoma, Mulamu Nghambi , Katibu wa zamani wa TFF, Michael Wambura, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Pitch invaders jailed for World Cup final act
17 Jul 2018, 11:15
English Premier League
What Sarri should do at Chelsea
14 Jul 2018, 15:50
Transfer News
BREAKING: Liverpool agrees deal for Roma goalkeeper
10 hours ago
Transfer News
BREAKING: Manchester United ace rejoins Ajax
17 Jul 2018, 13:20
Kenya Premier League
AFC Leopards to miss captain in Mashemeji Derby
2 hours ago