Masau Bwire: Kama sio uwanja Stand United hawangetufunga

Timu ya Ruvu Shooting imepoteza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Stand United kutokana na  hali mbaya ya uwanja wa CCM Kambarage Mkoani Shinyanga  na sio kucheza chini ya kiwango amesema Afisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire.

Ruvu Shooting ambao wamepoteza mchezo huo kwa kufungwa kwa  bao 1-0 na wenyeji Stand United wameutupia lawama uwanja wa Kambarage kuwa chanzo cha kichapo hicho.

Akizungumza na futaa.co.tz , Bwire amesema kuwa pamoja na kuwa mabeki wake kuzembea kidogo  kikwazo kikubwa kilisababishwa na uwanja huo  uliojaa matope na hivyo kuwafanya  wachezaji wake kushindwa  kuonesha ufundi wao licha ya Stand United kucheza chini ya kiwango dakika zote 90.

-Mchezo wakati fulani tunasema ni bahati, bahati haikuwa yetu wenzetu wakapata nafasi mabeki wetu wakazembea kidogo, uwanja pia haukuwa rafiki sana hatukucheza mpira tumepiga mpira laiti kama uwanja ungekuwa vizuri vijana wetu wangepata matokeo mazuri, amesema Bwire.

Bwire amesema kuwa kwa sasa wanaangazia mchezo ujao dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo Yanga utakaofanyika jijini Dar es Salaam huku akikiri kibarua kigumu kilichombele yao ni kurekebisha makosa madogo yaliyojitokeza katika michezo iliyopita.

-Tunajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Yanga, akili zetu na mawazo yetu yameelekezwa kwenye mchezo huo, tuna uhakika kwa sababu tutakuwa kwenye uwanja unaoeleweka mpira wetu utaonekana, amesema Bwire. 

Msimamo 

Kufuatia matokeo hayo hali ya  Ruvu Shooting inaendelea kudorora wakishika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi hiyo  wakiwa na alama 11 nao Stand United wakiendelea kuvuta  mkia wakiwa na alama 10 katika nafasi ya 15.

Related news
related/article
Local News
Njombe Mji: Yajayo dhidi ya Simba yawafurahisha
02 Apr, 16:49
Local News
AWCON 2018: She-Polopolo watua na mziki mnene kuwakabili Twiga Stars
02 Apr, 08:23
Local News
Azam Fc wakubali matokeo wahamishia nguvu kwenye ligi kuu
01 Apr, 19:45
Local News
ASFC: Singida United waangusha mbuyu, watinga nusu fainali
01 Apr, 18:10
Local News
ASFC: Stand United wajitapa kunyakuwa ubingwa
01 Apr, 12:03