Samatta apata pancha nyingine, Genk wakiichapa Zulte-Waregem

Samatta apata pancha nyingine, Genk wakiichapa Zulte-Waregem

10 Feb, 08:25

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania ambaye anakipiga kunako klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Ally Samatta maarufu kama Samagoals usiku wa Februari 10, ameshindwa kuendelea na mchezo na kulazimika kutolewa dakika ya 36.

Samatta akiichezea Genk dhidi ya timu ya Zulte-Waregem kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza ya Ubelgiji katika Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, alilazimika kutolewa baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo.

Samatta alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia kwa mara nyingine ikiwa ni siku chache tangu alipotoka kupona jeraha lake lililomfanya kufanyiwa upasuaji na kukaa nje ya uwanja kwa takribani majuma sita.

Bado daktari wa klabu hiyo hajatoa majibu ni muda gani Samatta atakuwa nje ya uwanja baada ya majeraha aliyoyapata katika mchezo ambao Genk ilishinda kwa mabao 3-1.

Ushindi wa 3-1

Mabao ya Genk katika mchezo yamefungwa na Nikos Karelis katika dakika ya 17, Thomas Buffel dakika ya 59, Alejandro Pozuelo katika dakika ya 90 huku lile la kufutia machozi la Zulte-Waregem likifungwa na Hamdi Harbaoui kwa njia ya penati katika dakika ya 32.

Mpaka sasa Samatta ameifungia KRC Genk mabao 22 katika michezo 75 ambayo amekwishaichezea akitokea TP Mazembe ya nchini Congo mwanzoni mwa mwaka 2016.

Related news
related/article
Local News
Okoth eyeing a top ten finish 
21 hours ago
International News
New era: Arsenal confirm new manager
23 hours ago
Local News
Lethal USM Alger's striker joins German side
23 May, 09:45
Betting Previews
UEFA CL Final preview: Real Madrid vs Liverpool-Prediction, team news & line-ups
23 hours ago
International News
WC 2018: Messi joins Argentina's training camp
22 May, 21:00