CAF CL: Msuva apiga hattrick, Difaa ikitoa kipigo kikali

CAF CL: Msuva apiga hattrick, Difaa ikitoa kipigo kikali

11 Feb, 00:11

Mtanzania Simon Msuva amefunga mabao matatu (Hat Trick) katika ushindi wa timu yake ya Difaa El Jadidi dhidi ya Benfica de Bissau ya Guinea-Bissau katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Difaa imeibuka na ushind mnono wa mabao 10-0 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Stade El Abdi El Jadida, nchini Morocco.

Msuva amefunga mabao yake katika dakika ya 56, 73 na 90 huku mabao mengine yakifungwa na Bakari N'Diaye na Hamid Ahaddad aliyefunga matano na Bilal El Magri akifunga moja.

Ushindi huo ndio mkubwa mpaka sasa katika michezo yote ya ligi ya mabingwa iliyofanyika kuanzia Ijumaa ya Februari 9 na Jumamosi ya Februari 10.

Related news
related/article
Local News
Kenya Premier League's game changers
15 hours ago
International News
Transfer talk: City eyes Kompany successor as Courtois delays contract talks
22 hours ago
Local News
AFC Leopards duo upbeat ahead of Harambee Stars friendlies
23 May, 10:20
International News
Rwanda to sponsor Arsenal's new sleeve
23 May, 11:05
International News
WC 2018: Messi joins Argentina's training camp
22 May, 21:00