CAF CC: 4G imesoma kwa Simba, Zimamoto wabanwa nyumbani

CAF CC: 4G imesoma kwa Simba, Zimamoto wabanwa nyumbani

11 Feb, 18:26

Timu ya soka ya Simba SC imeanza vyema michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmeria Tnanale ya nchini Djibouti.

Wakicheza kandanda safi katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Simba walipata bao la kwanza katika dakika ya kwanza tu ya mchezo kupitia kwa Said Hamisi Ndemla kwa faulo ya moja kwa moja nje kidogo ya 18.

Wakati mabao mengine matatu ya Simba yamefungwa na mkongwe John Raphael Bocco katika dakika ya 32, 45 na Emmanuel Okwi katika dakika 90 ya mtanange huo.

Aidha katika dakika ya 56 Gendarmerie walikosa penati kufuatia Abdulkarim Ahmed kufanyiwa faulo na Erasto Nyoni ndani ya 18, penati ambayo pengine ingewapa moyo wa kuendelea kupambana zaidi.

Kwa ushindi huo Simba watakuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kwani, kama Gendarmerie wanataka kufuzu basi itawabidi kushinda kwa mabao 5-0.

Hata hivyo Simba wamejihakikishia kushiriki hatua inayofuata na mshindi wa mchezo kati ya Green Buffaloes ya Zambia au El Masry ya Misri licha ya El Masry kushinda kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jumamosi Februari 10.

FT: Zimamoto 1-1 Welayta Dicha

Wakati huohuo maafande wa Zimamoto wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Welayta Dicha ya Ethiopia katika mchezo mwingine uliowakutanisha wawakilishi wa Tanzania upande wa Zanzibar katika michuano hiyo ya kimataifa.

Zimamoto ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 32 kupitia kwa Hakim Ali baada ya kupokea pasi kutoka kwa Yusuph Mtuba, kabla ya  Welayta Dicha kusawazisha kupitia kwa Arafat Djako kwa faulo ya moja kwa moja nje ya 18, katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar.

Matokeo Ligi Kuu:

FT: Njombe Mji 0-0 Mbeya City

FT: Singida United 0-1 Stand United

FT: Mbao FC 0-0 Mtibwa Sugar

FT: Ruvu Shooting 3-1 Lipuli FC

FT: Ndanda FC 0-0 Tanzania Prisons

Related news
related/article
International News
Real Madrid v Liverpool: Is the Champions League enough to save Zidane?
5 hours ago
International News
OFFICIAL: Arsenal release new home kit for 2018/19 season
7 hours ago
Transfer News
Transfer Talk: No offers from Chelsea or Zenit for Sarri
11 hours ago
International News
Spain announce 23-man FIFA World Cup squad
21 May, 15:50
International News
Messi: I like Griezmann
21 May, 08:30