CAF CC: Welayta Dicha, walia na Joto kali kuwanyima ushindi dhidi ya Zimamoto

CAF CC: Welayta Dicha, walia na Joto kali kuwanyima ushindi dhidi ya Zimamoto

12 Feb, 08:33

Mfungaji wa bao la kusawazisha la Welayta Dicha ya Ethiopia, katika mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Zimamoto FC Arafat Djako raia wa Togo, amesema kuwa hawajapoteza matumaini ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

Djako raia wa Togo amesema walikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo hali ya hewa ya Zanzibar ambayo amesema kulikuwa na joto nyingi tofauti na baridi walioizoea kwao Ethiopia, hata hivyo amesema  mchezo wa mpira  hautabiriki na chochote kinaweza kutokea.

"Sio matokeo mabaya sana kwetu na tuna amini tutafanya vyema, hali ya hewa ilituathiri hatujazoea joto kubwa, kwetu kuna baridi sana lakini tuna matumaini tukicheza nyumbani mambo yatakuwa tofauti tutafanya vizuri mchezo wa mpira hautabiriki", amesema Djako.

Djako amebainisha kuwa kipindi cha kwanza walitawaliwa zaidi kutokana na hali ya hewa lakini walirejea kipindi cha pili kwa nguvu baada ya jua kupunguza makali yake na kuanza kucheza soka walilolizoea.

Amesema cha muhimu ni kuwa wamepata bao la ugenini ambalo limewasaidia kwenda nyumbani wakiwa na Matumaini makubwa ya kusonga mbele.

Bao 1-1

Zimamoto ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 32 kupitia kwa Hakim Ali baada ya kupokea pasi kutoka kwa Yusuph Mtuba, kabla ya Welayta Dicha kusawazisha kupitia kwa Arafat Djako kwa faulo ya moja kwa moja nje ya 18, katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Amaan Visiwani Zanzibar.

Related news
related/article
Local News
Posta Rangers midfielder calls for suitors
18 hours ago
International News
UEFA CL: Road to Kiev
23 May, 19:00
International News
Guardiola hails new Arsenal boss
23 May, 17:30
International News
UEFA CL: Road to Kiev
23 May, 19:00
International News
UEFA Champions League final: Key players
23 May, 16:00