CAF CC: Djuma aukosoa mfumo wa Gendarmerie

CAF CC: Djuma aukosoa mfumo wa Gendarmerie

12 Feb, 08:51

Kocha msaidizi wa Timu ya Simba Mrundi Masoud Djuma amefurahia matokeo ya mchezo wa kwanza wa michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo walipata ushindi mnono na kusema kuwa itafanya mambo kuwa mepesi katika mchezo wa marudiano ambapo watakuwa ugenini.

Djuma ambaye ameukosoa mfumo wa kocha Arafat Djako na kuutaja wa kale ambao usioendana na soka ya sasa wakati Simba walitumia mbinu  na sio nguvu nyingi kama wapinzani wao kwani Simba bado wana michezo ya ligi ambayo pia inahitaji wakuwe katika hali nzuri.

"Wapinzani wetu hawakujipanga walitumia mifumo iliyopitwa na muda na ndio maana tuliwafunga sisi tulicheza kwa mpangilio hatukutumia nguvu nyingi na hatukuruhusu goli,tuna mechi nyingi mbele yetu na tunahitaji kuwa katika hali nzuri ili kushinda michezo yetu yote", amesema Djuma. 

Simba wamejihakikishia kushiriki hatua inayofuata na mshindi wa mchezo kati ya Green Buffaloes ya Zambia au El Masry ya Misri licha ya El Masry kushinda kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jumamosi Februari 10.

Related news
related/article
International News
Suarez: Iniesta hard to replace at Barcelona
22 hours ago
International News
Guardiola hails new Arsenal boss
23 May, 17:30
Local News
Harambee Stars to face New Zealand in Intercontinental Cup debut
23 May, 12:45
International News
Transfer talk: City eyes Kompany successor as Courtois delays contract talks
23 May, 13:00
Local News
Tanzanian giants trailing AFC Leopards midfielder
24 May, 07:50