VPL: Kagera Sugar, Azam walindiana heshima

VPL: Kagera Sugar, Azam walindiana heshima

12 Feb, 18:01

Ligi kuu soka Tanzania Bara raundi ya 18 mzunguko wa pili imeendelea Jumatatu ya Februari 12 kwa mchezo mmoja uliowakutanisha Kagera Sugar 'Wanankurukumbi' na Azam FC 'Wanarambaramba'.

Wakicheza katika dimba lenye nyasi bandia la Kaitaba mjini Bukoba, timu zimetoka sare ya bao 1-1, mabao yote yakipatikana katika kipindi cha pili cha mchezo huo.

Kimuhemuhe 

Azam hawakuwa vizuri kuanzia kipindi cha kwanza cha mchezo wakiruhusu kushambuliwa zaidi tofauti na matarajio ya wengi.

Kagera Sugar walipoteza nafasi mbili za wazi kuwapa nafasi ya kuongoza katika dakika 45 za mwanzo ikiwemo nafasi ya Jafary Kibaya ambaye aliweka kuwatoka mabeki wa Azam na kupigana shuti la kushtukiza ambalo ilibidi Razak alipooze Kabla ya kudaka tena.

Kibaya tena alipokea pasi ya Ally Ramadhan akiwa na nafasi ya kupiga free header lakini kwa mara nyingine kichwa chake kiliangalia Juu na kuutoa mpira nje kidogo ya lango la Azam.

Eladaus Mfubele 

Kipindi cha pili Kagera waliongeza kasi na kufanikiwa kupata faulo iliyochongwa na Jafary Kibaya.

Faulo hiyo tofauti na matarajio yake, mpira ulikatika na ukawa kama unatoka hivi ila ukamkuta mlinzi Eladaus Mfubele  na kuandika bao la kuongoza kwa Kagera Sugar.

Idd Kipagwile 

Bao hilo halikudumu sana kwani dakika ya 53 Azam walisawazisha bao hilo kupitia kwa Idd Kipagwile baada ya kumchambua Mwaita Gereza na kupiga shuti kali lililomshinda kipa Ramadhan Mohammed na kujaa wavuni.

Kagera wakicheza kandanda la kuvutia almanusura waandike bao la pili katika dakika ya 58, akiwa pekee yeye na golikipa Jafary Kibaya akashindwa kulenga lango na shuti lake ambalo alionekana kupania sana lilikatika na kwenda nje na kuwa mpira wa kurushwa.

Kagera waliongeza mashambulizi na katika dakika ya 63 walifanikiwa kuuzamisha mpira wavuni lakini bao hilo lilikataliwa kwa madai ya mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kuwa mfungaji alikuwa katika eneo la kuotea.

Dakika 90

Hadi kipyenga cha mwamuzi Emmanuel Mwandembwa kinapulizwa kuashiria dakika 90 kumalizika timu zote mbili Licha ya kosakosa za hapa na pale zilitoshana nguvu ya bao 1-1.

Matokeo hayo yanawafanya Azam FC kuendelea kukalia nafasi ya 3 wakiwa na alama 34 wakati Kagera Sugar wanakwea kwa nafasi moja hadi nafasi 15 wakiwa na alama 14 Sawa na Njombe Waliopo nafasi ya 16

Vikosi vilivyocheza.

Kagera Sugar: Ramadhan Mohammed 30, Mwaita Gereza 21, Eladslaus Mfulebe 2, Juma Shemvuni 25, Mohammed Fakh, George Kavila 15/ Peter Mwalyanzi, Seleman Mangoma 7, Ally Nasoro 6, Japhary Kibaya 4/ Edward Christopher, Ally Ramadhani 13 na Venance Ludovic 12/ Atupele Green.

Akiba: Said Kipao 18, Godfrey Taita 20, Peter Mwalyanzi 28, Paul Ngalyoma 8, Pastory Athanas 29, Atupele Green 3 na Edward Christipher 10.

Azam: Razack Abalora 16, Swaleh Abdallah 20/Enock Atta Agyei, Bruce Kangwa 26, David Mwantika 12, Yakub Mohammed 5, Abdallah Kheri 25, Stephan Kingue 27/ Paul Peter, Frank Domayo 18, Salmin Hozza 22, Mbaraka Yusuph 24/ Idd Kipagwile na Shaban Idd 43. 

Akiba: Mwadini Ally 1, Idd Kipagwile 21, Enock Atta 10, Benard Athur 9, Paul peter 51, Oscar Masai 47 na Masoud Abdallah 15.

Matokeo mengine VPL raundi ya 18.

FT: Njombe Mji 0-0 Mbeya City

FT: Singida United 0-1 Stand United

FT: Mbao FC 0-0 Mtibwa Sugar

FT: Ruvu Shooting 3-1 Lipuli FC

FT: Ndanda FC 0-0 Tanzania Prisons

Ratiba ya raundi ya 18.

Feb 14, 2018: Dar Young Africans v Majimaji

Feb 15, 2018: Mwadui FC v Simba SC 

Related news
related/article
Local News
AFC Leopards - Gor Mahia game called off
23 May, 21:40
Local News
Kenya Premier League's game changers
23 May, 19:20
International News
UEFA Champions League final: Key players
23 May, 16:00
International News
Guardiola hails new Arsenal boss
23 May, 17:30
Local News
Breaking: AFC Leopards appoints a new assistant coach
23 May, 08:10