| Futaa.com
General

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limekana tetesi ya kwamba kuna ubadhirifu wa fedha kama ilivyoripotiwa na wanahabari. 

Gazeti la Tanzanite lilichapisha ripoti jana (Disemba 10 2019) likidai kuna kashfa TFF ambapo zaidi ya milioni mia tatu zimetafunwa. 

TFF imekana madai hayo na kuchapisha kauli ambayo imesambazwa kwa wanahabari. 

Kauli ya TFF 

Shirikisho La Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kufafanua kuhusu taarifa kwa baadhi ya vyombo vya habari kuwa kumekuwa na ubadharifu wa fedha ndani ya TFF. 

Taarifa hiyo iliyochapwa kwenye gazeti la Tanzanite toleo namba 292 la Jumatatu Disemba 10, 2018, lenye kichwa cha habari KASHFA TFF, ZAIDI YA 300M ZATAFUNWA. 

Taarifa hio imejikita kwenye taarifa ya hesabu za TFF za mwaka 2015 na 2016 zilizopokelewa tarehe 11 Septemba 2016 na tarehe 27 Novemba 2017 kwa mfuatano na kufanyiwa kazi. 

Katika kipindi hicho kilichotajwa kimekuwa chini ya ukaguzi wa PCCB na tayari mashauri yako mahakamani yanaendelea ikiwa ni pamoja na kufuatiliwa waliotjwa katika hesabu za fedha katika kipindi cha mwaka wa 2015 na 2016. 

Kwa kuwa masuala hayo yapo kwenye ngazi ya mahakama, TFF inaona iviachie vyombo vya kisheria vifanye kazi yake kadiri ya taratibu zao.