Mfahamu Michael John Lema, Samatta mwingine anayekipiga Bundesliga.

Mfahamu Michael John Lema, Samatta mwingine anayekipiga Bundesliga.

30 Jul 2017, 17:43

Inawezekana miongoni mwa nchi mbazo zinawachezaji wengi wanaocheza nje ya Bara la Afrika kwa Upande wa Nchi za Afrika Mashariki Tanzania ikawa miongoni mwa zile zinazongoza.

Jina la Michael John Lema Linaweza kuwa miongoni mwa Majina ambayo ni mageni kabisa masikioni mwa Watanzania, lakini Mchezaji huyu anayecheza nafasi ya Kiungo ni kati ya Watanzania wachache wanaocheza soka katika ligi Zenye timu maarufu Duniani.

Mara kadhaa umeshawahi kusikia Timu kama Rapid Wien ambayo historia yake imejipambanua kwa kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya ama Uropa na kuleta Upinzani kwa vilabu vikubwa kama Manchester United na Paris Saint Germain.

Basi hizo ndio timu ambazo Mtanzania Michael John Lema atakutana nazo msimu huu pale atakapokuwa akiichezea Klabu ya SK Sturm Graz inayoshiriki ligi Kuu nchini Austria Maarufu kama Austrian Bundesliga.

Itigi, Singida.

Historia ya Michael Lema inaanza Miaka 17 iliyopita katika Mkoa wa Singida Maeneo ya Itigi Ambapo Mzee na Bibi John Lema waliweza kuleta Duniani Kiumbe ambacho kwa wakati huo pengine wasingeweza kujua kuwa wanamleta Mwanandinga Bora.

-Nimezaliwa Itigi Singida, Mimi nipo huku lakini wazazi wangu wote wapo Singida, Shule ya Msingi nilisoma hapohapo Itigi hadi Darasa la Nne ambayo ilikuwa ni mwaka 2009, ambapo nilikwenda Austria ambapo nilifikia kwa Rafiki wa mama Yangu, ambaye ndiye naweza kusema ni mfadhili wangu” Anaanza kusema Michael John Lema.

Michael anasema lengo kubwa la yeye kuchukuliwa kwenda Austria lilikuwa kwa ajili ya Masomo lakini kuna kipindi alipenda kwenda uwanjani kufanya mazoezi na huko ndipo kipaji chake kilipoonekana.

-Nilikuja huku kwa lengo la Masomo, lakini nilipofikisha miaka 10 nikaanza kuupenda mpira ambapo nilimuomba mfadhili wangu anipeleke uwanjani kufanya mazoezi ambapo nilicheza na wakaniona kuwa naweza kucheza vizuri, nakumbuka kuna siku  tulicheza na Sturm Graz ambapo kocha wao akaniona na kuniomba nijiunge na timu ya Watoto” Anasema.

Anajiunga na SK Sturm Graz.

Anasema baada ya kupigiwa simu mara ya kwanza alikataa lakini baada ya kama majuma mawili kocha wa timu hiyo alimpigia tena na hapo ndipo Akamuomba mlezi wake ampeleke Mji wa Graz ilipo academy ya Timu hiyo na kusaini Mkataba na Timu hiyo.

Michael ambaye kwa sasa yupo katika kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 17 cha Timu ya Taifa ya Austria anasema ndoto yake kubwa ni kuja kucheza Timu ya Taifa ya Tanzania kwani huko ndipo Nyumbani kwao.

-Nitafurahi sana iwapo siku moja nitaitwa katika Timu ya Taifa ya Tanzania, kwani Huko ndio Nyumbani kwetu, Wazazi wangu wapo huko, familia yangu na ndugu zangu wapo huko, ila shida ni kuwa tayari nimeshachukua uraia wa Austria lakini ikiwezekana kuitwa Taifa Stars nitafurahi sana” Anaongoza Kiungo Huyo.

Kucheza England.

Anasema ndoto yake kwa Ngazi ya Klabu ni kucheza Katika vilabu vikubwa vya Nchini England, kwani Tangu apandishwe kwenye Timu ya wakubwa Mapema Mwezi huu amekuwa akifanya mazoezi ya Nguvu ili kuweza kukuza Kipaji Chake.

-Natamani sana niingie Uwanjani nikiwa na Timu ya wakubwa hata nicheze dakika 2 tu nioneshe uwezo wangu, unajua baada ya miaka mitatu hadi mine nataka nionekane zaidi kimataifa na kucheza Ligi Kuu ya England na ninaimani kubwa kuwa hapo nitafika tu” Anasema.

Mchezaji huyo ambaye anavaa Jezi namba 38 katika Timu ya Sturm Graz alikuwapo katika kikosi cha akiba kwenye mchezo wa kufuzu kwa michuano ya Uropa Ligi dhidi ya Fenerbahçe ya Uturuki na kupoteza kwa mabao 2-1 mchezo uliopigwa Julai 27 Katika mji wa Graz Austria.

Michael John Lema ni Muafrika pekee katika Kikosi cha Timu Hiyo inayoshiriki ligi yenye Timu 10, Ligi ambayo Msimu wake ulianza Julai 22 Mwaka huu, na Timu hiyo Kushinda Mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya SKN Sankt Pölten huku mchezo wa Pili wakitarajiwa kucheza dhidi ya Austria Wien Jumapili ya Julai 30.

Related news
related/article
Mahrez, Sane & Jesus To Step Up In Aguero's Likely Absence
Futaa Best Bet
Mahrez, Sane & Jesus To Step Up In Aguero's Likely Absence
07 Dec 2018, 13:20
KPL release report on Western Kenya Stadia
Kenya Premier League
KPL release report on Western Kenya Stadia
2 hours ago
KIKO CUP: Gogo Boys book semi-final date with KNH
KIKO CUP: Gogo Boys book semi-final date with KNH
06 Dec 2018, 20:25
BREAKING: Manchester City midfielder out for three weeks
English Premier League
BREAKING: Manchester City midfielder out for three weeks
4 hours ago
CAFCL: Gor Mahia's clash against Lobi Stars rescheduled
CAF Champions League
CAFCL: Gor Mahia's clash against Lobi Stars rescheduled
7 hours ago