Samatta: Botswana ni Timu nzuri Lakini.....

Samatta: Botswana ni Timu nzuri Lakini.....

31 Aug 2017, 07:30
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta ameutaja mchezo wa Kirafiki dhidi ya Botswana kuwa mchezo mgumu kwani wapinzani wao ni wazuri.

Samatta amesema mara ya mwisho wanacheza na Botswana na Kuwafunga mabao 2-0 ulikuwa ni mchezo mgumu hivyo anaamini kabisa hali itakuwa hivyo siku ya Jumamosi.

-Botswana ni timu nzuri kwani hata mara ya mwisho walikuwa katika kiwango kizuri, walicheza vizuri na walitusumbua japo tulishinda, hivyo najua utakuwa ni mchezo mzuri kwa pande zote"

Samatta ameongeza kuwa Kukaa muda mrefu kwa kikosi na kufanya mazoezi pamoja kutasaidia timu hiyo kujijenga zaidi na kucheza soka zuri hiyo Jumamosi.

-Maandalizi yapo fresh,Timu inakaribia siku kama tatu au nne wakiwa kambini katika mazoezi, hivyo naamini tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo huo" Alisema Nahodha Huyo.

Kocha Salumu Mayanga.

Kwa upande wa Kocha Salumu Mayanga amesema kikosi chote kipo katika hali nzuri na wanaendelea vizuri katika mazoezi ambapo programu inaonesha wataendelea na mazoezi mchana wa Alhamis na Asubuhi ya Ijumaa kabla ya mchezo huo.

-Kwa kiasi kikubwa nisema asilimia 90 wachezaji wote wapo, mpaka muda huu tumebakisha wachezaji wawili tu ndio ambao hawajajiunga na timu, afya za vijana zipo vizuri na ni matumaini yangu tutaendelea na mazoezi vizuri" Alisema Mayanga.

Rekodi zinaonesha Botswana na Tanzania wamekwishacheza michezo Mitatu Tanzania wakishinda mchezo mmoja ambao Ulipigwa Machi 25 mwaka huu na Taifa Stars kuibuka na Ushindi wa mabao 2-0, huku michezo mingine miwili ikimalizika kwa Sare.
Related news
related/article
FIFA World Cup
Gareth Southgate hails England show
22 hours ago
Local News
Amulundu rejoins Zoo FC
14 Jun 2018, 20:10
Transfer News
Manchester United set record breaking price for Martial
8 hours ago
Transfer News
Arsenal agree fee to sign Leverkusen goalie
7 hours ago
FIFA World Cup
Cantona mocks Neymar haircut
10 hours ago