Kiungo wa Sony Sugar kuanza dhidi ya Botswana.

Kiungo wa Sony Sugar kuanza dhidi ya Botswana.

02 Sep 2017, 11:26

Kiungo wa Sony Sugar Fc ya nchini Kenya Abdallah Hamisi ameanza kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana.

Abdallah ameaminiwa na kocha Salumu Shabani Mayanga, ikiwa ni mara yake ya kwanza kuichezea Stars katika michezo ya Kimataifa, na amepewa majukumu ya kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji kama kiungo mchezeshaji.

Abdallah atasaidiwa na Mzamiru Yassin, Himid Mao Mkami, Shizya Kichuya na Simon Msuva katika kuhakikisha Stars inaibuka na ushindi katika mchezo huo utakaopigwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. 

Kikosi kamili.

Nafasi ya mlinda mlango ameanza Aishi Manula, huku walinzi wakiwa ni Erasto Nyoni, Gadiel Michael Mbaga, Abdi Banda, na Kelvin Yondani.

Viungo ni Himid Mao Mkami, Simon Msuva, Mzamiru Yassin, Shizya Ramadhan Kichuya na Abdallah Hamisi, Wakati Mbwana Ally Samatta atasimama kama mshambuliaji pekee katika kikosi hicho.

Wachezaji wa akiba

Mwadini Ally, Boniface Maganga, Raphael Daudi, Salim Mbonde, Said Ndemla, Aziz Bitegeko, Elius Maguri na Kelvin Sabato.

Related news
related/article
FIFA World Cup
Harry Kane the hero, as England stab resilient Tunisia
22 hours ago
FIFA World Cup
Dele Alli demands ruthless England approach
18 Jun 2018, 17:05
Transfer News
Southampton join the race to sign Arsenal ace
5 hours ago
International News
Another record! Second World Cup's quickest red card
6 hours ago
FIFA World Cup
Neymar limps out of training
3 hours ago