Mtanzania ajiunga na Mallorca ya Uhispania.

Mtanzania ajiunga na Mallorca ya Uhispania.

13 Sep 2017, 10:48

Mchezaji kinda wa Kitanzania , Prince Leonard mwenye umri wa miaka 17, amepata nafasi ya kwenda kujiunga na kituo cha Mallorca Toppfotball kilichopo nchini Hispania kwa ajili ya kuendelezwa kisoka, Mwanaspoti limeandika. 

Kituo hicho cha kibiashara kina wachezaji kadhaa ambao kimewauza kwenye timu kama Molde, Rosenborg, Brann, Strømsgodset, Sogndal, Assane, Torslanda, Sandnes Ulf, Drexel Dragons, Sandefjord na Bryne.

-Mzee wangu ananisapoti kwa kiasi kikubwa, muda mrefu kidogo nilimweleza kuwa nahitaji kuyatengeneza maisha yangu kupitia mpira. Safari yangu ni mwezi ujao,” alisema Prince.

Imethibitisha

Mallorca Toppfotball imethibitisha mapema mwanzoni mwa mwezi huu kupitia mtandano wa kijamii wa Facebook kuwa Prince atajiunga nao kwa msimu huu wa 2017/2018.

Kituo cha Mallorca Toppfotball kilianzishwa miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuzalisha vijana wenye misingi bora ya mpira ambao watakuwa na soko kwenye ushindani wa biashara ya soka

Related news
related/article
Local News
Gor Mahia to face Kenpoly at Machakos
9 hours ago
Local News
CECAFA Club: Ugandan giants eyeing glory in Tanzania
12 hours ago
FIFA World Cup
Preview: Poland vs. Senegal - Prediction, team news and lineups
8 hours ago
Local News
AFC Leopards signs Mathare United midfieder
4 hours ago
International News
Napoli star interested in Man City move
5 hours ago