WPL: Dirisha la usajili lafungwa, kupisha kipindi cha pingamizi.

WPL: Dirisha la usajili lafungwa, kupisha kipindi cha pingamizi.

13 Nov 2017, 16:07

Wakati Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikitarajiwa kuanza Novemba 26, 2017 katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, tayari usajili wa msimu kwa timu zote 12, umekamilika.

Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano, usajili ulipangwa ufanyike kati ya Oktoba 25 na Novemba 12, mwaka huu na kwamba kuanzia leo Novemba 13 hadi 17, mwaka huu ni kipindi cha pingamizi.

PNovemba 18, mwaka huu kutakuwa na kikao cha Kamati ya Sheria kabla ya Novemba 20, mwaka huu kutoa leseni za wachezaji. Novemba 24, mwaka huu kutakuwa na Semina ya Viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna jijini Dar es Salaam.

Ligi hatua ya makundi ikianza Novemba 26, mwaka huu ukomo utakuwa Desemba 9, mwaka huu na kupata jumla ya timu nane ambazo zitacheza ligi hatua ya Nane Bora ‘Super 8’ itaanza Desemba 20, mwaka huu kwa mfumo wa michezo ya nyumbani na ugenini.

Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.

Makundi kamili. 

Timu zilizosajili kutoka Kundi A ambazo ziko Dar es Salaam ni Simba Queens ya jijini Dar es Salaam iliyopanda daraja msimu huu, timu nyingine kwenye kundi hilo ni Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen zote za Dar es Salaam pamoja na timu za Fair Play ya Tanga na mabingwa watetezi Mlandizi Queens.

Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka kituo cha Dodoma, Marsh Academy pia ya Mwanza, Panama ya Iringa, Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens ya Singida.

Related news
related/article
International News
He is world class, Stuani hails Suarez
22 hours ago
Local News
Wazito parts ways with nine players 
23 Jun 2018, 13:50
FIFA World Cup
Honda's strike spoils Senegal's party
10 hours ago
Local News
Leopards power past Rain Forest in Naivasha
12 hours ago
FIFA World Cup
Lukaku breaks another record
23 Jun 2018, 16:35