Ligi Kuu: Simba wajichimbia Mbeya, kutafuta silaha ya kuwazima Prisons.

Ligi Kuu: Simba wajichimbia Mbeya, kutafuta silaha ya kuwazima Prisons.

14 Nov 2017, 09:22

Kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club kimeendelea na maandalizi ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu soka Tanzania dhidi ya Wajelajela Tanzania Prisons, ambapo kimeyataja maandalizi yao kuwa mazuri.

Simba bado wapo Jijini Mbeya baada ya safari katika mikoa ya Katavi na Rukwa ambapo kitakuwa jijini hapo hadi siku ya mchezo huo ambayo itakuwa ni Jumamosi ya Novemba 18 kwenye uwanja wa Sokoine.

Mratibu wa klabu ya Simba Abbas Ally, amesema wanafurahi kuwa maendeleo ya kikosi yapo vizuri na baada ya kucheza michezo miwili ya kirafiki imewasaidia kuwajenga zaidi kabla ya kukutana na Tanzania Prisons.

-Maendeleo ya kikosi chetu ni ya kuridhisha, tumecheza michezo miwili ya kirafiki mmoja tulitoka sare na Nyundo FC ya Katavi lakini mwingine tukashinda dhidi ya Rukwa Stars, hatuna mchezo mwingine wa kirafiki tunachoangalia sasa ni mchezo wetu dhidi ya Prisons,” ameeleza. 

Amesema kwa sasa maandalizi yao ni kuhakikisha wanafukia makosa yote yaliyotokea katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City ili kuhakikisha wanachukua alama Sita katika uwanja wa Sokoine msimu huu.

Historia inawabeba Prisons.

Ikumbukwe msimu uliopita Simba walipoteza katika uwanja huo dhidi ya Tanzania Prisons kwa mabao 2-1 na hicho kimezidi kuwafanya kuwa katika tahadhali kubwa dhidi ya Wajelajela hao.

-Mpira hauna historia, ukitaka kuleta historia hizo itabidi uwalete wachezaji wote waliotumika kwenye mchezo ule na kiukweli hilo haliwezekani kwani vikosi vimebadilika, kwa hiyo tunachoangalia tumecheza mechi yetu ya mwisho dhidi ya Mbeya City na tulishinda kwa bao moja, sasa kilicho mbele yetu ni kuhakikisha tunashinda katika mchezo unaokuja,” Abbas amesema.

Michezo mitano ya Simba iliyopita.

Stand United 1-2 Simba SC.

Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar.

Simba SC 4-0 Njombe Mji.

Yanga Sc 1-1 Simba SC.

Mbeya City 0-1 Simba SC.

Related news
related/article
Local News
Okiring hails giant killers, Falcons 
3 hours ago
Local News
Kahata, Tuyisenge score to keep Gor Mahia's unblemished run
23 Jun 2018, 16:55
FIFA World Cup
Sterling criticized by England legend
4 hours ago
FIFA World Cup
Nigeria striker terms Argentina clash as 'war'
7 hours ago
FIFA World Cup
Senegal regrets Japan draw, hopes for better results against Colombia
6 hours ago