Msuva afunguka kuhusu Kilimanjaro Stars na Yanga

Msuva afunguka kuhusu Kilimanjaro Stars na Yanga

05 Jan 2018, 11:25

Mshambuliaji wa Timu ya Difaa al Jadida ya Morocco na Timu ya Taifa, Simon Msuva, amekiri kuwa alisikitishwa na matokeo mabaya ambayo Timu ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' ilionesha katika mashindano yanayosimamiwa na baraza la vyama vya soka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’.

Katika mashindano hayo ambayo yalifanyika kuanzia Disemba 3-17 mwaka uliopita nchini Kenya huku Tanzania Bara wakiyaaga mashindano hayo katika hatua ya makundi, kwa kufungwa michezo mitatu na kutoka sare mchezo mmoja.

-kiukweli mimi kwanza kwa upande wangu kama mchezaji iliniuma kwa sababu nilikuwa nawasiliana kila siku na wachezaji wenzangu bans vipi inakuwa vipi,na nikaongea na captain akaniambia bana Simon sisi kama wachezaji tunashangaa tu matokeo yanakuwa hivi lakini ndo mpira na akaniambia kuwa hakuna matatizo mengine ila ni mechi tu zinawakuta wanapoteza", amesema Msuva.

Yanga watafanya vizuri?

Kuhusu mwenendo wa Yanga SC msimu huu mshambuliaji huyo wa zamani wa Timu hiyo amesema Yanga ni Timu nzuri na ambayo ina uwezo wa kufanya vizuri na kwa hivyo wasibezwe. 

-Yanga in Timu nzuri ni timu ambayo nimetoka Mimi kama mchezaji naamini in timu ambayo itafanya vizuri, naamini kina kitu kitafanyika ambacho watu wengi hawatakitegemea Yanga in timu nzuri ", amesema Msuva.

Msuva ambaye amerejea nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja na nusu amesema  atautumia muda huo kuwa karibu na familia yake.

Related news
related/article
International News
Costa delighted at Griezmann extension
3 hours ago
FIFA World Cup
Iceland: We have no magic formula to stop Messi
15 Jun 2018, 18:40
Local News
Shield Cup returns with Gor, Ulinzi kicking off second round
1 hour ago
International News
BREAKING: Wilshere announces Arsenal departure
10 hours ago
FIFA World Cup
First win for Africa as Senegal triumph
14 hours ago