Msuva: Nitacheza ulaya mwaka huu

Msuva: Nitacheza ulaya mwaka huu

06 Jan 2018, 12:18

Mshambuliaji wa Timu ya Difaa all Jadida ya Morocco na Timu ya Taifa Tanzania, Simon HappyGod Msuva amesema kuwa hajafikia malengo yake ya kisoka licha ya kuichezea klabu ya Morocco na kuwa malengo yake ni kucheza soka barani ulaya. 

Amesema ndoto yake ya kucheza soka ulaya ipo hai na kuwa Mungu akimjalia mwaka huu anaweza kuhamia ulaya.  

Akizungumza na futaa.co.tz Msuva amesema amejifunza vitu vingi nchini Morocco amesema ndoto yake IPO hai na kuwa Mungu akimjalia mwaka ujao atahimia ulaya.

-Nimecheza mechi 14 mpaka sasa nikiwa na Difaa mechi moja nimekosa, nina magoli matano na nimeweza ku assist magoli 3 kwa hiyo kitu ambacho kwa upande wangu ni mwanzo mzuri, nimejifunza vitu vingi kwa sababu kule wenzetu mpira wao upo tofauti sana na nitaendelea kujifunza na wengine", amesema Msuva.

Mfungaji bora. 

Mfungaji huyo bora wa ligi kuu msimu uliopita amesema nia yake ni kucheza Ulaya kwani bado yupo Afrika na kama ikibidi anaweza kwenda mwaka huu.

-Kila kitu kinakuwa na malengo yake, mimi pale nataka iwe kama transist niweze kutoka pale, bado nipo Afrika na nataka kuendelea zaidi kama Samatta na wachezaji wengine ambapo wapo ulaya naomba Mungu kila siku huu mwaka usiishe niweze kutoka ile sehemu na kwenda sehemu nyingine, dalili zipo, kuonesha mwenyewe juhudi zangu basi kila kitu kinawezekana", amesema Msuva.

Msuva ambaye alijiunga na Timu hiyo ya Morocco akitokea klabu ya Yanga SC amejihakikishia nafasi katika kikosi cha kwanza cha  timu hiyo kutoka na bidii yake uwanjani ambapo aliisaidia Difaa all Jadida kumaliza katika nafasi ya nne katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambayo ameitaja kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kuwepo kwa wachezaji walio na viwango vya juu.

Related news
related/article
FIFA World Cup
What went wrong for Brazil?
18 Jun 2018, 12:25
International News
Draxler backs exceptional Ozil to shine in Russia
17 Jun 2018, 09:00
International News
Pogba positive despite criticism, says Varane
1 hour ago
International News
Confirmed:Wilshere set to leave Arsenal
3 hours ago
International News
Costa delighted at Griezmann extension
3 hours ago