Tshishimbi atwaa tuzo ya VPL mwezi Februari

Tshishimbi atwaa tuzo ya VPL mwezi Februari

13 Mar 2018, 12:12

Kiungo wa Timu ya soka ya Yanga, Pappy Kabamba Tshishimbi amechaguliwa kuwa mcheza bora wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa mwezi Februari.

Katika mwezi Februari Tshishimbi Amecheza mechi zote nne ambazo timu hiyo ilicheza katika mfulululizo wa mechi za ligi na kufanikiwa kufunga mabao matatu na kutoa pasi ya bao moja. 

Walioshindana na Tshishimbi 

Walioshindana na Tshishimbi ni Pius Buswita wa Yanga, ambaye pia alichangia mafanikio hayo ya Yanga kwa mwezi huo, huku pia akifunga mabao mawili.

Mwingine aliyeingia hatua ya fainali ni Emmanuel Okwi wa Simba aliyeisaidia timu yake kupata pointi 10 kwa michezo minne, ikishinda mitatu na kutoka sare mmoja, huku Okwi akifunga mabao manne.

Raia huyo wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo atazawadiwa shilingi milioni moja pamoja na king'amuzi cha Azam kama zawadi ya kutwaa tuzo hiyo inayotolewa kila mwezi na kamati ya tuzo ya Shirikisho la Soka nchini (TFF).

Aidha Pappy Tshishimbi ambaye amesajiliwa na Yanga akitokea Mbabane Swallows ya Swaziland anakuwa mchezaji wa nne wakati kigeni kutwaa tuzo hiyo kwa msimu huu katika miezi saba ambayo tuzo hiyo imeshatolewa.

Wachezaji wengine ambao tayari wametwaa tuzo ya mwezi kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi (Agosti), Shafiq Batambuze (Septemba), Obrey Chirwa (Oktoba), Mudathir Yahya( Novemba) na Habibu Haji Kiyombo (Disemba).

Related news
related/article
Local News
Waithera starts, Nyakha on the bench for Nakumatt- Homeboyz showdown
18 hours ago
Local News
Zoo, Sony share spoils in dramatic draw
16 Jun 2018, 17:10
FIFA World Cup
Evra defends Pogba
10 hours ago
FIFA World Cup
Ronaldo matches Pele, Puskas' records
16 Jun 2018, 09:05
Local News
Indeche on target as Nakumatt humiliates Kakamega Homeboyz
15 hours ago